Na Emmanuela Yogolelo
Je! Umewahi kugundua kitu chochote kingine kuhusu muziki badala ya muziki kuwa sauti hizi za kupendeza na sauti nzuri?
Mimi nimegunduwa tayari.
Wewe pia? Basi kama umekwishakugunduwa, utujulishe maoni yako kupita nafasi ya commentaire.
Nimegundua kuwa kuna mila ambazo zinafanywa karibu ya muziki. Mamoja zaonekana kuwa za kisanaa zaidi na mengine kidogo ila vyote ni viungo ambavyo hufanya muziki iwe muziki.
Barani Afrika ambapo ninatoka, mila hizo ni nyingi na tofauti. Mamoja zabadilika na mengine hazibadilike. Mila za muziki za kiafrika zinanivutia na kuhamasisha ubunifu na Kazi zangu.
Mila kuu za muziki au viungo barani Afrika ni nyimbo/sauti, juchera/densi na ‘percussion’. Katika muziki wa kiafrika, haya matatu hayawezi kutengwa.
Mila mingine ya muziki wa kiafrika ni ‘major’, ‘minor’ na ‘pentatonic’; nyimbo na sauti; vifaa/vyombo vya muziki; mwitikio-wito; ‘harmonies’; midundo ifuatayo na mwendo; ‘chanting’ na ‘humming’; ‘ululation’; hadisi; ‘improvisation’; ‘dramatisation’ na uchangamano na ushiriki. Nitazungumuza zaidi juu ya mila moja au mbili katika chapisho linalofuata na kabla ya kufunua muziki wetu mpya wa Afro-Raga.
Nawaacha hapa leo na sampuli/mifano chache za midundo zifuatano na mwendo (‘Rythm’) huko DR Congo, katika mkao wa kati wa Afrika.
Kwa midundo ya Agwaya pia ‘Kalalila’, sıkıya KILIYO YA MAMA AFRIKA
https://soundcloud.com/search?q=emmanuela%20yogolelo
Kwa midundo zaidi ya Agwaya/Kalalila na Soukous/Seben, sikiya AMANI @ LUSH
Kwa midundo ya Rumba, sikiliza MAKOLO YA MASSIYA
Endelea kutembelea blog hii juu uelewe miradi mingine nitakayokuwa nikifanya katika siku zijazo. Nitapakua ujumbe zaidi hapa; nyimbo ninaandika; maonyesho ambayo ninafanya na masomo ya jumla yanayohusiana na taaluma yangu.
Hivi karibuni nitaweza kutoa huduma zangu za kawaida na zingine mpya piya mdondoni. Ada inategemeya Viwango vya Muungano Wanamuziki.
Huduma ninazotoa sasa ni :
Warsha za kuimba za Kiafrika
Mafunzo katika utumiaji wa mila ya muziki ya Kiafrika kama mbinu ya kuunda vipande vya maingiliano na maonyesho
Vipindi vya uboreshaji na mimi karibu na uimbaji wa Kiafrika, uandishi wa nyimbo na uimbaji wa polyphonic / maonyesho.
Kwa habari zaidi juu ya huduma hizi au maoni, tuma barua pepe kupitia ukurasa wa mawasiliano, email. sremmanuela@googlemail.com wala piga 07868591070
Hadi wiki ijayo, tafadhali jiandikishe kwenye blogi hii (KWENYE HOME PAGE, CHINI); likes, gabuwa, amabiya marafiki kuusu hii blog na uacha maoni yenye kujenga.
Asante.