Na Emmanuela Yogolelo
Jinsi tunasemaka kwa Kiswahili ya kwetu Kivu (mashariki mwa DR Kongo) ‘leo njo leo’, basi, leo na njoo ile siku tulingozeya.
Ushirikiyano wangu na Jaydev umemalizika, na kazi ni nzuri sana. Basi nimefurahi kuwatolea mwimbo na muziki wa kwanza wa Afro-Raga ambao tumeunda pamoja. Sehemu ndogo wa wimbo wetu ilichezwa kwenye Radio ya BBC, Front Row Jumatano iliyopita usiku. https://www.bbc.co.uk/programmes/m000ktyp
Natumai utapenda na tafadhali imba, cheza, piga chombo unayo pamoja nasi!
Kabla ya kufanya hivyo, acha niwape mafasiriyo kuhusu mila ya muziki wakiafrika tumetumiya katika muziki na wimbo uhu.
Gambo ya mila ya muziki wa Kiafrika tumetumiya: ‘humming’; ‘chanting’; wimbo; jibu simu; ‘harmonies’; maneno na vigelegele.
Gambo ya mila ya muziki ya India, tumetumiya Raga (‘scale’ wala ‘mood’) Bairagi Bhairav iliyochezwa kwenye bomba la Bansuri (filimbi ya mianzi ya India). Hii imeonyeshwa wazi katika ‘Alap’, ambayo ni sehemu ya ufunguzi. Vyombo vingine ni pamoja na sanduku la Tanpura na Shruti, ambalo hutoa sauti za sauti zilizopo katika muundo wote. Mtazamo mkubwa wa kipande hicho ni Tabla inayoungwa mkono na vipande mbali mbali vya sauti vinavyotumika kwenye sehemu ndogo ya India.
Jamaa, nimeaimba kama mwenye kuvunja mironyororo kwa Sehemu ya ‘intro’ na katikati wa wimbo.
Mwimbo wetu unaitwa “Dunia”. Neno Dunia inamaanisha ulimwengu katika lugha langu la swahili. Dunia inaweza pia kumaanisha wanadamu na hata maisha.
Jaydev usema kama neno Dunia imeandikwa na kusomwa “Duniya” na inamaanisha piya ulimwengu katika lugha Hindi.
Nimesikia pia kama neno ili “Dunia “, iko kwenye lugha ya Kiarabu na imemaanisha piya ulimwengu (Ni kweli ? Kama unajuwa, basi utujulishe katika sehemu ya maoni/comments).
Katika wimbo wetu, ‘Dunia’ inamaanisha ulimwengu, wanadamu na maisha.
Basi, iyi ndiyo maneno na tafsiri ya mwimbo wetu:
Ah Dunia, Dunia, Dunia Ni Mambo Dunia – Ah Dunia, Dunia, Dunia Ni Mambo Dunia
Ah Dunia, Dunia, Dunia Hadisi Dunia – Ah Dunia Dunia Dunia Hadisi Dunia 2x
Dunia Ni Mambo – Dunia Ni Mambo
Dunia Hadisi – Dunia Hadisi 2x
Eeh Eeeh, Eeh Eeeh 2x
KWA KUSIKILIZA VIZURI UHU MWIMBA, TUMIA SPEAKERS/HAUT PARLEURS INAYO BASSI.
Endelea kutembelea blog hii juu uelewe miradi mingine nitakayokuwa nikifanya katika siku zijazo.
Nitapakua ujumbe zaidi hapa; nyimbo ninaandika; maonyesho ambayo ninafanya na masomo ya jumla yanayohusiana na taaluma yangu.
Hivi karibuni nitaweza kutoa huduma zangu za kawaida na zingine mpya piya mdondoni. Ada inategemeya Viwango vya Muungano Wanamuziki.
Huduma ninazotoa sasa ni:
Warsha za kuimba za Kiafrika
Mafunzo katika utumiaji wa mila ya muziki ya Kiafrika kama mbinu ya kuunda vipande vya maingiliano na maonyesho.
Vipindi vya uboreshaji na mimi karibu na uimbaji wa Kiafrika, uandishi wa nyimbo na uimbaji wa polyphonic / maonyesho.
Kwa habari zaidi juu ya huduma hizi au maoni, tuma barua pepe kupitia ukurasa wa mawasiliano, email. sremmanuela@googlemail.com wala piga (0044)7868591070
Hadi wiki ijayo, tafadhali jiandikishe kwenye blogi hii (KWENYE HOME PAGE, CHINI); nifuate kwenye Twiiter (Emmanuela Yogolelo wala @emmanuelayogol1) likes, gabuwa, amabiya marafiki kuusu hii blog na uacha maoni yenye kujenga.
Asante.